I made this widget at MyFlashFetish.com.

code-matuwille

MPENZI MSIKILIZAJI WA MBEYA FM, PENDEKEZA WIMBO UNAOONA UNAFAA KUINGIA KWENYE TOP 30, KABLA YA JUMAPILI AU TUMA MAONI YAKO KUPITIA 0757762963

2011

WAJANJA WA TOWN

WASIKILIZE WAJANJA WA TOWN KUPITIA 89.5 MBEYA FM....PRESENTER-VICE PRESIDENT NA SMART BOY

September 18, 2010

Mshindi Project Fame kuzoa Milioni 95/-

Vijana watatu wa Kitanzania watashiriki katika fainali za mashindano ya mwaka huu ya kusaka vipaji vya kuimba ya Tusker Project Fame, ambayo mshindi wa kwanza atapata zawadi ya Sh. Milioni 95. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), Teddy Mapunda, alisema kuwa jumla ya washiriki 15 kutoka katika nchi tano za Afrika Mashariki na Kati watashiriki katika hatua ya fainali.

 
Teddy alizitaja nchi zitakazotoa washiriki wa mashindano hayo kuwa ni pamoja na Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Sudani Kusini. Wawakilishi kutoka kila nchi wataingia katika kambi maalumu Septemba 25.

Alisema kuwa kwa Tanzania, usaili wa kuwapata washiriki hao utafanyika kesho kwenye hoteli ya Peacock, jijini Dar es Salaam.

Aliongeza kuwa lengo la kampuni yake kudhamini mashindano hayo ni kwa ajili ya kuendeleza na kuinua vipaji vya wasanii vijana wa nchi hizo tano.

Alisema kuwa vijana wanaotakiwa kushiriki ni wa kuanzia umri wa miaka 23 na kuendelea na kusisitiza kwamba baada ya wawakilishi wa Tanzania kupatikana, wadau wa sanaa hiyo watatakiwa kuwapigia kura ili wasitolewe mapema katika mchakato wa kumpata mshindi.

Naye Meneja Matukio wa SBL, Bahati Singh, aliwataka vijana wote wanaojua kuimba, wajitokeze kuwania nafasi hiyo ya kuendeleza ndoto zao.

Alisema kuwa mbali na zawadi ya fedha atakayopata mshindi, vile vile wadhamini hao wanatoa nafasi ya kwenda kurekodi albamu ya muziki nchini Afrika Kusini.

Aliwataja majaji watakaosimamia mchujo wa kesho kuwa ni Hamisi Bakari, Paul Ndunguru na Sauda Simba Kilumanga.

Muimbaji Nakaaya Sumari na Hemed, ambaye siku hizi amekuwa nyota wa filamu za Tanzania, ni miongoni mwa wasanii walioibuliwa na mashindano hayo.

Fomu kwa ajili ya kujiandikisha kushiriki shindano hilo zinatolewa bure katika sehemu mbalimbali nchini.
 

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni yako hapa chini

TANGAZA NASI KWA BEI NAFUU.., WASILIANA NASI 0757762963

TANGAZA NASI KWA BEI NAFUU.., WASILIANA NASI 0757762963
Matangazo hayo pia yatarushwa moja kwa Moja Kupitia 89.5 MBEYA FM Radio.!!