May 20, 2011
BREKING NEWSSSSSSSSS : Sheikh Yahya Hussein afariki dunia Leo
Marehemu Sheikh Yahaya Hussein enzi za uhai wake
Habari ambazo tumezipata hivi Punde zinasema kwamba mnajimu maarufu Sheikh Yahya Hussein amefariki dunia.
Mtoto wa marehemu, Hassan Yahya Hussein, kaithibitishia Globu ya Jamii sasa hivi kwamba baba yake amefariki dunia mnamo saa nne asubuhi ya leo nyumbani kwake Mwembe Chai jijini Dar es salaam. Alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya moyo.
Hassan amesema mipango ya mazishi yanafanyika hapo hapo Mwembe Chai, na kwamba maziko yanatarajiwa kufanbyika kesho hapo nyumbani kwa marehemu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni yako hapa chini