Kiama kilitakiwa kiwe Jumamosi saa 12 jioni lakini hakikutokea kama kilivyotabiriwa na mchungaji Harold Camping wa nchini Marekani ambaye alitumia pesa nyingi sana kuwaonya watu kwa miezi kadhaa kuwa kiama kingetokea jana May 21,2011
Wafuasi na waumini wa Mchungaji Harold Camping wamebaki hawajui la kufanya baada ya kuhubiriwa kwa miezi mingi kuwa kiama kingetokea jana jumamosi saa 12 jioni,huku familia moja ilisafiri kilomita 4830 toka Maryland hadi California mbele ya ofisi ya radio ya mchungaji Camping na kusubiri kupaishwa mbinguni kwenda kuonana na Yesu huku Mzee mmoja wa miak 60,Robert Fitzpatrick kwa kuamini kuwa mwisho wa dunia umefika na kwa kuamini mafundisho ya mchungaji Camping,alitumia dola $140,000 toka kwenye akiba yake ili kuchapisha mabango na vipeperushi vya kuwaonya watu kuwa mwisho wa dunia ni May 21 Mchungaji Camping mwenyewe hajaonekana tena na amekaa kimya na hadi sasa hajasema chochote kwanini kiama hakikutokea kama alivyotabiri na kuwahabarisha watu kwa miezi kadhaa kabla,hata hivyo bado waumini wengine wa mchungaji Camping wanaendelea kumuamini mchungaji huyo wakisema kuwa kuchelewa kutokea kwa kiama ni mtihani mwingine toka kwa Mungu juu ya imani zao
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni yako hapa chini