Tanzania kuna mababu, mabibi na hata vijana wanaotoa huduma za vikombe kwa imani ya kuwaponya watu maradhi yao, nchini Indonesia watu wanalala juu ya reli za treni kwa imani magonjwa waliyo nayo yataondoka mara moja.
Si kitu cha ajabu kuona watu wakiwa wamelala kwenye reli za treni kwenye jimbo la Java nchini Indonesia.
Watu hufanya hivyo kwa imani kwamba nishati hafifu ya umeme inayopatikana kwenye reli inaweza kuyatibu maradhi yoyote yale.
Imani hiyo imewafanya watu wengi kujilaza kwenye reli za treni kwa masaa mengi ambapo wengine hudiriki kulala hapo siku nzima.
Tofauti na huduma za vikombe zinazotolewa Tanzania ambapo mgonjwa huchangia kidogo cha fedha, huduma hii ya tiba kwa kujilaza kwenye reli ni ya bure hivyo watu wengi wenye kuamini watapona kwa kujilaza kwenye reli wamekuwa wakifanya hivyo.
Treni zinapokuwa zikipita kwenye reli, huduma ya uponyaji husimamishwa kwa muda na pindi treni zinapokuwa zimeshaipita watu hurudi tena kujilaza kwenye reli.
Imani hiyo imezidi kuvuta watu wengi baada ya baadhi ya watu kudai wamepona magonjwa yaliyokuwa yakiwasumbua.

No comments:
Post a Comment
Toa Maoni yako hapa chini