I made this widget at MyFlashFetish.com.

code-matuwille

MPENZI MSIKILIZAJI WA MBEYA FM, PENDEKEZA WIMBO UNAOONA UNAFAA KUINGIA KWENYE TOP 30, KABLA YA JUMAPILI AU TUMA MAONI YAKO KUPITIA 0757762963

2011

WAJANJA WA TOWN

WASIKILIZE WAJANJA WA TOWN KUPITIA 89.5 MBEYA FM....PRESENTER-VICE PRESIDENT NA SMART BOY

September 16, 2011

PIGO KUBWA MBEYA

Ajali na Maafa Nchini yanazidi kushika Kasi,Kama Sikosei Hii ni mara ya Tatu kusikika Kuungua kwa Masoko Mkoani Mbeya., la Kwanza ni SOKO LA MWAJELWA,SOKO LKA UHINDINI na Sasa ni SOKO LA SIDO/Mwanjelwa.!
zifuatazo ni Baadhi ya Picha katika hekeheka za Uokoaji mali

Eneo la Tukio Moto ukishika Kasi pasipokujulikana ZimaMoto walipo


Hekaheka za Uokoaji wa Mali
Moja ya Wafanyabiashara aliyeunguliwa Mali zake akiwa Amezimia baada ya Mshtuko Mkubwa wa Kuona Mali zake zikiteketea
Mali zimebaki Majivu
Upande wa Pili sehem ambapo Soko jipya linajengwa kukiwa kumejaa Umati Mkubwa wa Watu
Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani Ezekiel Mgeni akitoa Maelezo Jinsi gani wanajitahidi Kudhibiti Kutokea kwa Ajali Eneo hilo,
SIDO Upande mwingine


Moja ya Mfanyabiashara akiwa amejuruhiwa na Kitu chenye Ncha Kali kichwani wakati akiokoa Mali zake
                                     Zimamoto ikiwasili kwa Kasi Eneo la Tukio

                                        Gari la Jiji likiwa Eneo la Tukio pasipo kumwaga Maji kwenye Moto

Mshike Mshike

Kiasi kidogo cha Mali zilizo okolewa huku zingine zikiibwa na Kuungua kabisa na Moto
Soko la SIDO likiacha Historia
Baadhi ya Mali zilizo Okolewa
Umati wa Wananchi Eneo la Tukio
Baadhi ya Wafanyabiashara wakishuhudia Mali zao zikiteketea


September 14, 2011

PIRIKA PIRIKA ZA MBEYA

Ajali ya Ndege Ndogo ikitoka Mbeya kuelekea Mradi wa Kapunga 

                                      Nyomi ya Watu eneo la Kilimo Uyole wakishuhudia Ndege hiyo                                                     

                                         Kaimu Kamanda Polisi Mkoa wa Mbeya akizungumza na Wanahabari                                           
                                           Kitu kikiwa Chini ya Ardhi(Kiwanja kisicho Rasmi)

                                                       Wanahabari Kazini

                                      Askari wa Usalama wakihakikisha Hali inaenda sawa


                                           Muonekano wa Ndege kwa Mbele huku Kioo kikiwa kimevunjika


                     Rubani wa Ndege  hiyo akitoa Maelezo kwa Mbeya FM na www.wakalinext.blogspot.com

                                         Hon;Stanslaus Lambat eneo la Tukio..,



                                      Wanambeya wakiwa wanafuatilia Tukio zima



ENEO LA HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA

Askari wa Jiji la Mbeya wakitoa Plate Numbers kwenye Magari yanayoegeshwasehemu zisizoruhusiwa
 
                                       Hapa Jamaa alikuwa ananizuia Eti mpaka niwaombe Ruhusa ya kupiga Picha
                                           Haya nimepata Ruhusa.., Mgambo Kazini
 Ukiitazama Vizuri picha hii utaona kibao chenye Alama inayoashiria Hairuhusiwi kuegesha Gari eneo hili

NB; Haki zote zimehifadhiwa;Habari hii mara utakapo ichukua hakikisha Unaonesha Mtandao huu uliochukua www.wakalinext.blogspot.com

September 10, 2011

AJALI MBAYA ZANZIBAR., MELI YA SPICE YAZAMA

Meli ya LCT Spice Islanders ikiwa imezama Pwani ya Nungwi.



Meli ya LCT SPICE ISLANDERS imebinuka na kuzama katika Bahari ya Hindi huko Pwani ya Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja ikielekea Pemba.

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu, Mh Issa Haji Ussi akithibitisha tukio hilo amesema ajali  imetokea milango ya saa 8:30 za usiku wa kuamkia leo, na kuongezea kuwa  meli hiyo ilikuwa imebeba abiria 610 pamoja na mizigo.


Mh Ussi  amesema meli hiyo iliyokuwa imeondoka katika Bandari ya Malindi Unguja ikiwa katika hali ya uzima, lakini katikati ya safari ikapata hitilafu na kusababisha kubiruka na hatimaye kuzama.
Hadi sasa haijaweza kufahamika idadi kamili ya watu waliofariki,lakini vyombo vya uokozi vimefika katika eneo la tukio kutoa msaada.

Naibu Waziri  huyo  amesema Serikali kwa kushirikiana na vyombo vya usafiri vya binafsi  vya boti ziendazo kasi zimekwenda eneo la tukio kutoa msaada unaohitajika, huku Jeshi la Polisi Tanzania limetuma Helikopta yake kwenye eneo la tukio.

Awali, amesema Mamlaka zinazohusika zilipata taarifa za kuzama kwa meli hiyo baada ya Meli ya Mv Jitihada inayomilikiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuripoti kuzama kwa meli ya Spice Islanders ambayo ililazimika kukatisha safari yake kuelekea Kisiwani Pemba na kwenda kwenye tukio.

Serikali imesema taarifa zaidi zitakuwa zikitolewa na wananchi wameombwa kuwa watulivu.

Kwa Habari zaidi endelea kutembelea Mtandao wetu

September 09, 2011

Stanslaus Lambat Umjuaye..,

Yeaah.!! Ni kwamba Jamaa kitambo kidogo tangu afiche Makucha na Maujanja yake ya Ukweli awapo kwenye Programmz, so Story ni kwamba kwa sasa Jamaa ameonekana kujipanga zaidi na kuja kwa kasi ya Ajabu sanaaaa though yeye mwenyewe hajafunguka Lakini Kitaa kimesound hivyo kutokana na Kasi aliyoanza nayo tangu wiki hii Ianze

Hon;Stanslaus Lambat (Presenter's Vice President)
Haijajulikana mara Moja kwanini jamaa alikaa kimya kidogo ila Tetesi ni kwamba kutokana na Kuona aliowaachia nafasi hawaitumii vizuri nafasi hiyo so cha Muhimu tune 89.5 Mhz Mbeya FM all the Tym hususani Jumamosi saa Moja Asubuhi mpaka saa Tatu, Jumapili Saa Tatu mpaka saa Saba kwenye Rasha rasha za Top 30 na Jumanne saa Moja mpaka Tatu asubuhi.!!! Lol, dats ma Men Lambat

September 06, 2011

MKUTANO WA HADHARA WA MHESHIMIWA MBUNGE WA MBEYA MJINI MH. JOSEPH MBILINYI MAENEO YA SIDO MWANJELWA TAREHE 5-9-2011

Mh. sugu akipokelewa na Maelfu ya Wananchi kwa shangwe

Asalaaaaaam..!!!

Mh. Peter Msigwa nae akiwasili


Makamanda wa CHADEMA wanaopigania Haki za Watanzania wakiketi tayari kwa Mkutano

Maelfu ya Watu Upande wa Kaskazini

Upande wa Magharibi


Mashariki nako hakukuwa na Njia ya Kupitika

Upande wa Barabarani nako ni Mshikemshike


Viongozi mbalimbali wa Chama na Wananchi wakiwa Wanafuatilia kwa Makini kila kinachoendelea


John Mwambgija maarufu kwa jina la Mzee wa Upako akimkaribisha Ndugu Fred Mpendazoe Kuwasilim Wakazi wa Mbeya..,

Mpendazoe akihutubia wakazi wa Mbeya

"Tutashinda" Kitabu hiki kilinunuliwa sana na Wakazi wa Mbeya.., Ni Kitabu kilichotungwa na Fred Mpendazoe chenye kuelezea Mambo mbalimbali yenye kuifanya Nchi ipate Mwelekeo Mzuri

Fred Mpendazoe Kazini


Mch. Peter Msigwa Mzee wa Weaper akitoa Salam kwa Wananchi wa Mbeya



Wiper zenye Kuashiria Umoja na Mshikamano zikaanza..,  Kuliaaaa

Kushotooooo





Ni Nomaaa.., Msigwa alitikisa Jiji kwa Style yake ya Wiper kama inavyoonekana.!


Mh. Sugu akipanda Jukwaani tayari kwa Kuzungumza na Maelfu ya Wananchi wa Jimbo la Mbeya Mjini

Mh. Joseph Mbilinyi akisisitiza Jambo

Wananchi wakimshangilia kwa Furaha Mbunge wao ambaye alikuwa akitoa Salam za Bungeni

Sugu Kazini

MASWALI NA MAONI KWA MBUNGE/ SALAM ZA WANANCHI KWA MBUNGE

Kijana Alex Fednand amabaye alikuwa najihusisha na Biashara ya Umachinga akitoa Ushuhuda wa Jinsi alivyokamatwa na Askari na kupotezewa Mali zake

Mzee Yesaya Mwakajile alimuomba Mbunge wa Mbeya Mjini amsaidie kupata Haki ya Mafao baada ya Kustaafu, alikuwa anafanya Kazi Wizara ya Afya

Mwanafunzi wa Sekondari ya Mt. Aggrey alimuomba Mh. Sugu asaide swala kukuza Vipaji Mashuleni ambalo kwa sasa limesahaulika kwa kiwango kikubwa pamoja na Kompyuta.., Mheshimiwa Sugu alisema swala la vipaji mashuleni ni moja ya Sera zake na litatatuliwa huku akimuhakikishia kwa Upande wa Kompyuta kuwa anamalizia Mazungumzo na Kampuni ya SAMSUNG ili kompyuta hizo zije mara moja,
Dada Mwanaharakati kama alivyojitambulisha aligusia Swala la Bank ya Wanawake na NGO'S za Kitapeli zinazoanzishwa Mkoani Mbeya...,Mh. Sugu alimuahidi kuwa kuna Mpango kabambe wa kuanzishwa Community Bank Mkoani Mbeya hivyo itawanufaisha Wananchi wengi wa Mbeya pia Alikemea uwepo huo NGO'S feki kama ilivyolezwa na kuzitaka ziache mara moja

Mama huyu alimulezea Sugu Jinsi Kesi yake iliyodumu kwa zaidi ya Miaka 7 na Jinsi asivyotendewa Haki hivyo anaomba Msaada, Mh. Sugu alimuomba afike Ofisini ili wajue wapi wataanzia kutatua Tatizo hilo

Ndugu A.C Mzee wa Jiji alipanda Jukwaani kwa Niaba ya Wakazi wa Jiji la Mbeya kumpongeza Mbunge wa Mbeya Mjini kwa Jinsi anvyojituma kuwa karibu na Wananchi ili kujua Changamoto zinazowakabili ingawa ni muda mfupi sana tangu ameingia Madarakani..,

Mh. Sugu akiondoka huku Umati Mkubwa wa Wananchi ukitaka walau kumuona kwa Ukaribu na Kumshika Mkono, palikuwa hapapitiki.!! huyu ndiye Sugu wa Vijana, Wazee,Watoto na kila Mtu.!!

BAADHI YA MAMBO ALIYOYAZUNGUMZIA MH. SUGU KWENYE MKUTANO HUU

Mheshimiwa Joseph Mbilinyi alizisifu Juhudi za Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Bwana. Jumanne Idd ambaye wanashirikiana Pamoja kwa Nia ya kuhakikisha Mbeya inasonga Mbele kimaendeleo

  • Atolea Ufafanuzi juu ya Tv Mbeya ambayo kwa sasa wapo kwenye Mchakato ili ianze kurusha Matangazo yake kwa Nyanda za Juu Kusini

  • Asema ni Lazima kwa kipindi hiki cha Uongozi wake ahakikishe Matatizo ya Maji yanatatuliwa na Barabara ya LAMI kwa Kilomita 29 ni Lazima Ijengwe.
Aelezea Wazo lake la Kuanzishwa kwa Mchezo wa Jackpot Jijini Mbeya lenye nia kukuza Kipato kwa Wananchi na Serikali ili kukwepa Adha ya Kukusanya Michango kwa Wananchi
Awaomba Madiwani ambao wanaamini maeneo yao yanfaa kwa Uchimbaji wa Mabwawa ya Samaki wapeleke Majina ya Kata zao ili Miradi hiyo mianze mara moja
  • Atoa Wazo la kuwepo kwa Kombe la MBUNGE kwenye Michezo mbalimbali ikiwemo Football, pia Nia ya Kuanzaishwa kwa Mapambano mbalimbali ya Ngumi. 
  • Ahidi Ujenzi wa Taa za Barabarani ni Lazima Ukamilike
Ahidi kuendelea kwa Tamasha la Burudani Nyumbani lenye nia kukuza Vipaji na Kuwapa Fursa Wafanya Biashara mbalimbali kuuza Bidhaa zao wakati wote wa Tamasha hilo.

TANGAZA NASI KWA BEI NAFUU.., WASILIANA NASI 0757762963

TANGAZA NASI KWA BEI NAFUU.., WASILIANA NASI 0757762963
Matangazo hayo pia yatarushwa moja kwa Moja Kupitia 89.5 MBEYA FM Radio.!!