Mh. sugu akipokelewa na Maelfu ya Wananchi kwa shangwe
Asalaaaaaam..!!!
Mh. Peter Msigwa nae akiwasili
Makamanda wa CHADEMA wanaopigania Haki za Watanzania wakiketi tayari kwa Mkutano
Maelfu ya Watu Upande wa Kaskazini
Upande wa Magharibi
Mashariki nako hakukuwa na Njia ya Kupitika
Upande wa Barabarani nako ni Mshikemshike
Viongozi mbalimbali wa Chama na Wananchi wakiwa Wanafuatilia kwa Makini kila kinachoendelea
John Mwambgija maarufu kwa jina la Mzee wa Upako akimkaribisha Ndugu Fred Mpendazoe Kuwasilim Wakazi wa Mbeya..,
Mpendazoe akihutubia wakazi wa Mbeya
"Tutashinda" Kitabu hiki kilinunuliwa sana na Wakazi wa Mbeya.., Ni Kitabu kilichotungwa na Fred Mpendazoe chenye kuelezea Mambo mbalimbali yenye kuifanya Nchi ipate Mwelekeo Mzuri
Fred Mpendazoe Kazini
Mch. Peter Msigwa Mzee wa Weaper akitoa Salam kwa Wananchi wa Mbeya
Wiper zenye Kuashiria Umoja na Mshikamano zikaanza.., Kuliaaaa
Kushotooooo
Ni Nomaaa.., Msigwa alitikisa Jiji kwa Style yake ya Wiper kama inavyoonekana.!
Mh. Sugu akipanda Jukwaani tayari kwa Kuzungumza na Maelfu ya Wananchi wa Jimbo la Mbeya Mjini
Mh. Joseph Mbilinyi akisisitiza Jambo
Wananchi wakimshangilia kwa Furaha Mbunge wao ambaye alikuwa akitoa Salam za Bungeni
Sugu Kazini
MASWALI NA MAONI KWA MBUNGE/ SALAM ZA WANANCHI KWA MBUNGE
Kijana Alex Fednand amabaye alikuwa najihusisha na Biashara ya Umachinga akitoa Ushuhuda wa Jinsi alivyokamatwa na Askari na kupotezewa Mali zake
Mzee Yesaya Mwakajile alimuomba Mbunge wa Mbeya Mjini amsaidie kupata Haki ya Mafao baada ya Kustaafu, alikuwa anafanya Kazi Wizara ya Afya
Mwanafunzi wa Sekondari ya Mt. Aggrey alimuomba Mh. Sugu asaide swala kukuza Vipaji Mashuleni ambalo kwa sasa limesahaulika kwa kiwango kikubwa pamoja na Kompyuta.., Mheshimiwa Sugu alisema swala la vipaji mashuleni ni moja ya Sera zake na litatatuliwa huku akimuhakikishia kwa Upande wa Kompyuta kuwa anamalizia Mazungumzo na Kampuni ya SAMSUNG ili kompyuta hizo zije mara moja,
Dada Mwanaharakati kama alivyojitambulisha aligusia Swala la Bank ya Wanawake na NGO'S za Kitapeli zinazoanzishwa Mkoani Mbeya...,Mh. Sugu alimuahidi kuwa kuna Mpango kabambe wa kuanzishwa Community Bank Mkoani Mbeya hivyo itawanufaisha Wananchi wengi wa Mbeya pia Alikemea uwepo huo NGO'S feki kama ilivyolezwa na kuzitaka ziache mara moja
Mama huyu alimulezea Sugu Jinsi Kesi yake iliyodumu kwa zaidi ya Miaka 7 na Jinsi asivyotendewa Haki hivyo anaomba Msaada, Mh. Sugu alimuomba afike Ofisini ili wajue wapi wataanzia kutatua Tatizo hilo
Ndugu A.C Mzee wa Jiji alipanda Jukwaani kwa Niaba ya Wakazi wa Jiji la Mbeya kumpongeza Mbunge wa Mbeya Mjini kwa Jinsi anvyojituma kuwa karibu na Wananchi ili kujua Changamoto zinazowakabili ingawa ni muda mfupi sana tangu ameingia Madarakani..,
Mh. Sugu akiondoka huku Umati Mkubwa wa Wananchi ukitaka walau kumuona kwa Ukaribu na Kumshika Mkono, palikuwa hapapitiki.!! huyu ndiye Sugu wa Vijana, Wazee,Watoto na kila Mtu.!!
BAADHI YA MAMBO ALIYOYAZUNGUMZIA MH. SUGU KWENYE MKUTANO HUU
Mheshimiwa Joseph Mbilinyi alizisifu Juhudi za Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Bwana. Jumanne Idd ambaye wanashirikiana Pamoja kwa Nia ya kuhakikisha Mbeya inasonga Mbele kimaendeleo
- Atolea Ufafanuzi juu ya Tv Mbeya ambayo kwa sasa wapo kwenye Mchakato ili ianze kurusha Matangazo yake kwa Nyanda za Juu Kusini
- Asema ni Lazima kwa kipindi hiki cha Uongozi wake ahakikishe Matatizo ya Maji yanatatuliwa na Barabara ya LAMI kwa Kilomita 29 ni Lazima Ijengwe.
Awaomba Madiwani ambao wanaamini maeneo yao yanfaa kwa Uchimbaji wa Mabwawa ya Samaki wapeleke Majina ya Kata zao ili Miradi hiyo mianze mara moja
- Atoa Wazo la kuwepo kwa Kombe la MBUNGE kwenye Michezo mbalimbali ikiwemo Football, pia Nia ya Kuanzaishwa kwa Mapambano mbalimbali ya Ngumi.
- Ahidi Ujenzi wa Taa za Barabarani ni Lazima Ukamilike
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni yako hapa chini