Kiba na kolabo la mastar US !
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Ali Kiba, amekisanua kwenda mjini Chicago, Marekani kurekodi wimbo utakaowahusisha nyota kadhaa wakiwemo Mnigeria 2Face Idibia, Fally Ipupa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Amani wa Kenya.
Waandaaji wa safari ya msanii huyo, kampuni ya Rockstar 4000, walisema kuwa Ali Kiba ataungana na ‘mastaa’ nane wa Afrika kurekodi wimbo huo, wakiwa pia na nyota mmojawapo wa muziki nchini Marekani ambaye bado hajatajwa.
Akizungumza jana Dar, mwakilishi wa Rockstar 4000, Christina Mosha ‘Seven’, alisema kuwa mafanikio ya Ali Kiba katika muziki wake wa kizazi kipya ndiyo yaliyombeba na kumpa nafasi ya kwenda Marekani kurekodi wimbo na nyota wengine wa Afrika.
“Huu ni mpango wa muda mrefu, ukiwa na lengo la kuwatambulisha wanamuziki wetu wa Afrika nje ya mipaka ya bara letu,” alisema Seven.
Alisema wasanii wengine watatoka katika nchi zaGabon , Ghana , Zambia na Uganda .
Akizungumza jana Dar, mwakilishi wa Rockstar 4000, Christina Mosha ‘Seven’, alisema kuwa mafanikio ya Ali Kiba katika muziki wake wa kizazi kipya ndiyo yaliyombeba na kumpa nafasi ya kwenda Marekani kurekodi wimbo na nyota wengine wa Afrika.
“Huu ni mpango wa muda mrefu, ukiwa na lengo la kuwatambulisha wanamuziki wetu wa Afrika nje ya mipaka ya bara letu,” alisema Seven.
Alisema wasanii wengine watatoka katika nchi za
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni yako hapa chini