Mtoto huyo alizaliwa katika jimbo la Sichuan akiwa na viungo vyote kamili kama watoto wengine isipokuwa alikuwa na vichwa viwili.
Kwa mujibu wa shirika la habari la China, mtoto huyo alikuwa na mabega mapana ambapo vichwa viwili vilijitokeza kwenye mabega yake.
Taarifa zaidi zilisema kuwa mtoto huyo alikuwa na mikono miwili, miguu miwili na viungo vingine vyote kamili.
Daktari aliyekuwa akiwaangalia watoto hao alisema kuwa ni vigumu sana kwa mtoto huyo kuweza kuishi muda mrefu kutokana na jinsi maumbile yake yalivyoungana.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni yako hapa chini