Namtambulisha kwenu mwanamke dada jasiri, msomi na mpenda maendeleo, mwenye kuamini kuwa maendeleo yoyote ya mwanamke yanakuja kwa juhudi zake mwenyewe, hekima, umakini, busara, uvumilivu na heshima na sio tu kusubiri kubebwa au uwezeshwaji tu kama inavyotafsiriwa na baadhi ya watu wengi nchini juu ya wanawake. Dada huyu ni mama wa watoto wawili wa kiume na ni mzaliwa wa Mbeya.
Huyu si mwingine bali ni Dakta Mary Mwanjelwa, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya kutokea CCM.
Mary Mwanjelwa ambaye amewahi kuwa Meneja Mradi 'Liason Manager' wa iliyokuwa Afrika Mashariki Gold Mine, baadae Placer dome ambayo sasa inaitwa Africa Gold Barrick (kampuni ya madini), na pia kabla hajawa Mbunge alikuwa ni Mkurugenzi wa Corporate wa Population Services International (PSI Tanzania) Shirika linalotoa huduma ya Afya ya jamii.
Mhe. Mary ambaye ana Shahada ya Uzamivu (PHD) ya Heshima kwenye Humanity toka Chuo Kikuu huko California, Marekani, pia ana Shahada ya Uzamili kwenye masuala ya Mawasiliano toka Chuo Kikuu cha St. Augustine, Mwanza-Tanzania, pia ana Stashahada ya Juu ya Uzamili katika masuala ya Uhusiano wa Kimataifa na Kidiplomasia toka katika Chuo cha Uhusiano wa Kimataifa na Diplomasia cha Kurasini, DSM-Tanzania Vile vile ana Stashahada ya Juu ya Diploma kwenye Business Administration.
Mary aliyesomea shule ya Msingi Muungano, Sekondari ya Sangu zote za jijini Mbeya, na baadaye Sekondari ya Siha -Moshi; anasema Elimu ni ufunguo na haina mwisho.
Dkt. Mary anaamini kuwa Baba wa Taifa, Hayati Mwl. Nyerere ndie aliyemvutia sana kuingia katika siasa na anaishi kupitia yale aliyoagiza na kutusii tuyafuate na kuyaenzi, hivyo mwaka 2005 alijitosa katika kinyang'anyiro cha Ubunge akafika kwenye tatu bora za mkoani kwake na kuingia kwenye 'kapu' kama wanavyoita UWT lakini kwa bahati mbaya kura hazikutosha lakini hakukata tamaa aliendelea kuomba nafasi mbalimbali katika chama chake cha CCM na kufanikiwa kupata nafasi zote alizoomba katika chama.
Dkt. Mary Mwanjelwa ambaye ni Mwanamke anayependa kufanya kazi kwa bidii na Kusoma siku zote, mcheshi na makini, mcha Mungu lakini 'principled' aliamua kuingia kwenye Siasa ili kutumika vema kwa nchi na wananchi akiwapeperushia bendera, kuwawakiilisha na kuwa karibu nao zaidi kwani anaamini katika mabadiliko kuendana na wakati pia.
Dkt. Mary Mwanjelwa ambaye ni Mwanamke anayependa kufanya kazi kwa bidii na Kusoma siku zote, mcheshi na makini, mcha Mungu lakini 'principled' aliamua kuingia kwenye Siasa ili kutumika vema kwa nchi na wananchi akiwapeperushia bendera, kuwawakiilisha na kuwa karibu nao zaidi kwani anaamini katika mabadiliko kuendana na wakati pia.
Dada huyu aliyekamilika katika nyanja nyingi, ukimuangalia kwa haraka haraka waweza kusema utamuingiaje pengine anajidai n.k, lakini ukweli ukishamfahamu kwa undani hakika Mungu amemjalia mengi.
Huyu ndiye Dakta Mary Mwanjelwa,Msomi ambaye ni makini kwa kumsikiliza kila Mmoja pasipo ubaguzi.! hapa akihojiana naMoja ya Waandishi wa Habari.! Yupo karibu na Kila Mwananchi ili aweze kuwa Msemaji mzuri wa kila Mwenye shida katika kutatua Matatizo yanayowakabiri Wananchi Mbunge wa Viti Maalum CCM Mbeya Mjini Dakta Mary Mwanjelwa akimkabidhi Katibu wa UWT wilaya ya Mbeya mjini, Sarah Mgoli, msaada wa shati zenye nembo ya CCM kwa ajili ya wajumbe wa Baraza la UWT wilayani humo. Misaada ni sehem ya Maisha yake Huyo ndiye Mary Mwanjelwa anayewasihi Wanawake wajenge upendo, Umoja na Mshikamano baina yao na kuondoa dhana Mbaya ya Adui wa Mwanamke ni Mwanamke mwenyewe, huku akiwasihi Wanawake wa Mkoa wa Mbeya kujishughulisha zaidi kwani wana sifa ya uchapaji kazi hivyo wajitume.!! |
Nzuri sana
ReplyDelete